Soka saa 24!

Video: Simba ya sasa haitaki tena kushindana na Yanga wala kupigania ligi kuu peke yake bali makombe yenye hadhi – Manara

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Haji Manara amesema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa klabu na ule wa Uchaguzi yamekamilika na hivyo kuwataka wanachama kujitokeza kwa wingi siku Jumapili 4/11/2018 ili wachague Mwenyekiti wa klabu na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Manara amewataka wanachama kuhakikisha wanachagua viongozi ambao wanaamini wanauwezo wa kuisaidia Simba kusonga mbele ili iweze kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

“Simba ya sasa inahitaji viongozi ambao wataifanya Simba licha ya kujiendesha kiuchumi lakini iweze kupigania makombe yenye hadhi ikiwepo klabu bingwa Afrika.Wawe watu wenye mipango ya kuipeleka Simba mbele, lazima tuliangalie hilo, amesema Manara.

Haji Manara ameongeza “Sasa hivi mnaona tumeanza ujenzi wa uwanja, Simba sasa ina wachezaji wakubwa, Simba sasa ina watu wakubwa, tuchukue watu ambao wataichukua Simba 2018 hadi 2022 angalau tushinde klabu bingwa ya Afrika,” amesema Manara.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW