Burudani

Video: Smile adai Bongo Flava haipewi uzito Zanzibar

Msanii anayefanya vizuri kwa sasa kisiwani Zanzibar, Smile amebainisha kuwa muziki wa Bongo Flava haupati nafasi kisiwani humo licha ya kuwa na wasanii wakubwa.

Smile

Akiongea na Bongo5, Smile anayetamba na ngoma yake ya ‘Saa Ngapi’ ameeleza kuwa muziki wa watu hao maarufu umefanikiwa kutokana na kuwa wanaimba muziki wa nyumbani amabo ni mduara.

“Nafikiri muziki wa kina AT wao ulikuwa ume base kinyumbani nyumbani mduara, wakila Berry walitoka kwa sababu radio na Tv zilikuwa chache sana, ndiyo maana nimesa kuwa utandawazi sasa hivi umekuwa unakuta radio nyingi Tv nyingi na wasanii wengi ndiyo maana tunachelewa kwa vingi,” amesema Smile.

Akaongeza kuwa “Sababu ya kuchelewa ni kwenye ku-push na hakuna watu wanaoweza ku-support wala kampuni wanoweza kuwekeza kupitia wasanii, unakuta wasanii wengi tuna watu wachache sana na mpaka usafiri uende Dar ukutane na mtu aweze kukusaidia.”

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents