Michezo

Video: Tazama Documentary ya Everton nchini Tanzania

Klabu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imeandaa Documentary inayoonyesha ziara yao ya siku mbili hapa nchini Tanzania.

Everton ambayo iliwasili nchini siku ya Jumamosi ya Julai 12 mwaka huu ilipata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo jijini Dar es salaam na kushiriki michezo tofauti tofauti na watoto wenye ulemavu wa Usikivu na Uoni  hafifu.

Kushiriki katika mazoezi ya pamoja na timu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino United) mazoezi yaliyo fanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam

Lakini pia walifanya kliniki kwa vikosi B vya timu za Yanga SC, Simba SC pamoja na Academy ya watoto katika viwanja vya Gymkhana.

Julai 8 mwaka huu klabu hiyo yenye maskani yake nchini Uingereza ilimtanguliza Nguli na balozi wa The Toffees  mchezaji mkongwe, Leon Osman hapa nchini na kufanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo makaburi ya Jumuiya ya Madola yaliyopo eneo la makumbusho kwa kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya jumuiya Madola.

Leon alipata nafasi ya kutembea juu ya daraja linaloshikiliwa na kamba ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Manyara. Lakini pia alipata  zawadi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Manyara pamoja Bendera ya Tanzania na kumpa heshima ya kuwa balozi wa Utalii Tanzania.

Julai 13 mwaka huu Everton wakahitimisha ziara yao kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Sportpesa Super Cup klabu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo uliyochezwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na wageni hao kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Gor Mahi.

Katika mchezo huo uliyovuta mashabiki wengi na wadau wa soka ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents