Burudani

Video: Tazama producer T-Minus alivyoipika ngoma ‘Blem’ ya Drake

Kwa miaka mingi staa wa muziki kutoka Canada na anayeishi Marekani maarufu kama Drake, amejenga uhusiano na mtayarishi wa muziki wa nchini kwao mwenye makazi mjini Toronto T-Minus.

T-Minus amekuwa kwenye mstari wa mbele katika safari ya muziki ya staa na rapper mkali duniani. Na alihusika kwenye kutengeneza hits za Drake zikiwemo The Motto, HYFR, Make me Proud na Replacement Girl. Japo T-Minus ameonekana mkimya kwa miaka michache iliyopita, lakini yeye ndiye producer aliyepewa sifa zote baada ya kukamilika kwa album mpya ya Drake, More Life.

Nikinukuu baadhi ya maneno kwenye ukanda huu mfupi wa video anasema, “Huwezi kujua vile Drake atachukua. Huwa namtumia kila kitu. Mara tu ninaposikia Drake anaandika ama anatumia beat kuandikia muziki mpya, huwa ni habari nzuri kwangu kuzipata kutoka kwakwe kwasababu yeye ndiye msanii mkali kushinda wote wale ambao nimeshawahi kufanya kazi nao. Hapo ndio utajua kuwa wimbo utakuwa hit kwa jinsi unaweza kwabma tu kusikiliza beat jinsi ilivyo tamu na kuimba melodi zake. Hujikuta nimeropoka kuwa hii iko sawa.”

Hebu burudika kwa kutazama producer huyu mkali kutoka Toronto nchini Canada anavyotumia software ya Fruity Loops kuipika ngoma Blem hapa chini.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents