Habari

Video: Tazama tukio la mnyama ‘Dolphin’ akizaa majini, kisha akaanza kumfundisha mtoto wake aliyezaliwa kuogelea

Kamera imefanikiwa kurekodi video ya mnyama wa majini dolphin akizaa mtoto (calf) na kisha akaanza kumuonesha jinsi ya kucheza na maji ikiwa ndio siku ya kwanza mtoto huyo dolphin anaingia duniani.

dolphine

Dolphin huyo mdogo alizaliwa majira ya saa 5 asubuhi Ijumaa iliyopita (Aug 2) huko Brookfield Zoo, Chicago, Marekani masaa mawili baada ya dolphin mja mzito mwenye miaka 26 kuanza kuonesha dalili za kukaribia kuzaa.

Katika video hiyo utaona dolphin (pomboo) mwenye mimba akiwa anatanga tanga majini (kama ishara ya uchungu) huku dolphin mwenzake akiwa karibu naye kumpa msaada wakati wa kuzaa, na ghafla mtoto akaanza kutoka mkia wakati anazaliwa.

Tazama video

http://youtu.be/mXLvq7DxJzY

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents