Michezo

Video: Tazama Wachezaji wa Simba wakisherehekea ubingwa wa VPL

Wachezaji wa Mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba wameonekana kuanza kusherehekea ubingwa wao baada ya Yanga kuvuliwa rasmi hapo jana na timu ya TZ Prisons kwa jumla ya mabao 2 – 0 dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Nyota hao wa Wekundu wa Msimbazi simba wakiwemo, Emmanuel Okwi, John Bocco, Shiza kichuya, Erasto Nyoni na wengine wameonekana kushangiria wakiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya kupata matokeo ya hasimu wao Yanga kuwa amepoteza mchezo wake dhidi ya TZ Prisons.

Yanga yenye pointi 48 ilihitaji kushinda michezo yake yote huku akiiyombea dua baya Simba kupoteza walau mechi moja ili kujihakikishia kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo hali ambayo imekuwa tofauti baada ya kukubali kipigo hicho mbele ya Prisons.

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba mpaka sasa inajumla ya pointi 65 huku ikisaliwa na michezo mitatu mkononi kabla ya kumaliza msimu huu wa mwaka 2017/18.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents