Videos

Video: Tediah Josiah arejea kuvionesha njia ya kutoka vipaji vya sanaa vya Afrika Mashariki

Producer mkongwe wa muziki wa nchini Kenya, Tediah Josiah alikuwa kimya kwa muda mrefu lakini sasa anarejea tena kwa kishindo. Tayari ameshaanzisha studio yake mpya iitwayo Sand Stone Studio, S3.

Pamoja na hivyo, Ted ameanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo na maelekezo kuhusu muziki kwa vijana wenye nia kufika mbalii kwenye sanaa ya muziki na video kupitia video anazorekodi na kupost kwenye Youtube.

“The reason to set up this studio was so that we can have a base as artists to exchange ideas, come and record music, come and share different things that we are trying to do and looking at getting real quality out of Kenya at least for now,” anasema Tedd kwenye video hiyo.

“Because I feel we have some great ideas but sometimes the quality kuna vile inalegea, mixing imekuwa ni mbaya or the lyrics, the vocals are… mtu ameandika tu kuhusu jana usiku inspiration inakuwa imechapa ukuta, those kinds of things, I don’t wanna do that anymore, I want to be able to inspire people to a point where mtu aanze kufikiria ‘how do I write a love song in real poetry and in real Swahili. How do I use the language that is already there instead of pretending to be a guy from South Central of New York because you are not. Kusema ukweli umetoka hapa Kenya, kama umetoka hapa Kenya do kitu ya hapa Kenya, kitu ya maana, kitu ya nguvu.”

Tedd Josiah ambaye mwanzo alikuwa na studio iitwayo Blu Zebra Records alikimbilia nchini Uingereza mwaka 2008 kutafuta hifadhi ya kisiasa kutokana na maisha yake kuwa hatarini nchini humo.

Tedd ambaye pia ni muongozaji na mtayarishaji wa video alitengeneza tangazo la TV lililojulikana kama Domo TV ambalo lilidaiwa kuwa la uchochezi kati ya chama cha ODM na PNU kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.

Mtayarishaji huyo alirejea nchini Kenya mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents