Michezo

Video teknoloji (VAR) yainufaisha timu ya taifa ya Uingereza (Picha+Video)

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate anaamini video technology (VAR) haiwezi mara zote kukupatia majibu sahihi kwa asilimia mia hii imekuja mara baada ya mchezo wa kirafiki uliochezwa jana dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane akipewa kadi nyekundu

Katika mchezo huo Uingereza ilipata goli la penati kupitia mfumo wa teknolojia baada ya kung’amua mchezaji Raphael Varane kumchezea ndivyo sivyo Dele Alli katika eneo la penati boksi na hivyo Varane kuzawadiwa kadi nyekundu.

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa  Ufaransa ikishinda magoli 3 kwa 2 ya Uingreza 

Southgate alisema, “Mi nadhani muamuzi alihitaji kuhakikisha na kwa kufanya hivyo yalikuwa maamuzi ya busaran bado si jambo la kuamini sana.”

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane akishinda goli la pili katika mchezo wao na Ufaransa

Katika mchezo huo timu ya taifa ya Ufaransa iliifunga Uingereza kwa jumla ya magoli 3 kwa 2 licha ya wenyeji hao kucheza pungufu katika kipindi chapili kwa kuwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya Raphael Varane kutolewa kwa kadi nyekundu.

https://youtu.be/3-hLJYkCf3w

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents