Burudani

Video: Trailer ya filamu ‘12 Years A Slave’ ya Mkenya Lupita Nyong’o aliyoigiza na Brad Pitt

Hii ni trailer ya filamu mpya ya Hollywood, ‘12 Years A Slave’ ambayo ameigiza pia muigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o anayejulikana kama Patsey kwenye filamu hiyo.

12 Years a Slave inatokana na kitabu cha historia kilichoandikwa na Solomon Northup, Mmarekani aliyetekwa na kuuzwa kama mtumwa.

Filamu hii imeongozwa na Steve McQueen na kuandikwa na John Ridley huku muigizaji Chiwetel Ejiofor akiigiza kama Solomon Northup. Waigizaji wengine kwenye filamu hiyo ni pamoja na Brad Pitt, Michael Fassbender,Benedict Cumberbatch,Paul Dano, Paul Giamatti.

12 Years a Slave inatarajiwa kuingia sokoni October 18, 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents