Habari

Video: Trailer ya movie mpya ‘WINNIE MANDELA’ iliyochezwa na Jennifer Hudson na Terrence Howard nchini Afrika Kusini (HD)

Hii ni Official Trailer ya movie iliyokuwa ikisubiriwa muda mrefu iitwayo ‘WINNIE MANDELA’ iliyochezwa na mastaa wa Marekani Jennifer Hudson na Terrence Howard.

Katika movie hii mwimbaji wa R&B Jennifer Hudson ameigiza kama mke wa zamani wa Madiba Winnie Mandela, huku Terrence Howard ameigiza kama mzee Nelson Mandela, Wendy Crewson kama Mary Botha pamoja na Elias Koteas kama Colonel DeVries. Movie imefanyika nchini Afrika Kusini.

Movie ya ‘Winnie’ inaelezea maisha ya aliyekuwa mke wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela (Jenniffer Hudson) hasa baada ya mumewe Nelson Mandela (Terrence Howard) kufungwa, ikionesha manyanyaso aliyoyapata kutoka kwa polisi na ugumu wa maisha.

‘Winnie’ imeshutiwa katika majiji ya Johannesburg, Cape town na Robben Island nchini Afrika Afrika Kusini kuanzia April 2010.

Kwa mujibu wa Wikipedia Mama Winnie Mandela (halisi) aliikosoa movie hiyo kwa kusema kuwa swala la wahusika kwenda mpaka Afrika Kusini na kushoot movie inayohusu maisha yake bila yeye kupewa taarifa huku bado yuko hai ni kumdharau.

“I have absolutely nothing against Jennifer [Hudson, the film’s star], but I have everything against the movie itself. I was not consulted. I am still alive, and I think that it is a total disrespect to come to South Africa, make a movie about my struggle, and call that movie some translation of a romantic life of Winnie Mandela.” Alisema Winnie

Movie ya Winnie iliyoandaliwa na Image Entertainment inategemewa kutoka rasmi mwezi ujao (September 6).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents