Michezo

Video: Tukio hili lamuweka Conor McGregor chini ya uchunguzi mkali wa Polisi

Mpiganaji wa MMA, Conor McGregor amejikuta akiwa chini ya uchunguzi wa jeshi la polisi la jijini New York (NYPD) baada ya kuvamia kikao cha baadhi ya wapiganaji wa UFC  na waandishi wa habari hapo jana siku ya Alhamisi huko Brooklyn na kufanya vitendo vya vurugu hadi kupelekea kuvunja kio cha basi lililokuwa limewapakia wapambanaji hao.

https://youtu.be/3Kg7OYe_Iu8

Rais wa UFC, Dana White amelitaka jeshi la polisi na EMS kumkamata mpiganaji huyo, McGregor ambaye amijizoelea umaarufu mkubwa ulimwenguni tangu alipo pambana na Floyd Mayweather.

Msemaji wa NYPD amekiambia chombo cha habari cha RTE News kuwa mpaka sasa wanaendelea kumtafuta McGregor ili kuzungumza nae na wale wote waliyohusika katika ghasia hizo zilizotokea Barclays centre huko Brooklyn.

Tukio hilo limetokea wakati wapiganaji wa MMA wakiwa na mkutano na vyombo vya habari kuelekea pambano lao huku rais, Dana White akisisitiza kuwa tukio lililofanywa na mpiganaji huyo halikubaliki hata katika historia ya kampuni hiyo.

McGregor raia wa Ireland amefanya vurugu hizo baada ya kuandaliwa kwa pambano kati ya Max Holloway na Khabib Nurmagomedov ambalo watapigania mkanda wa UFC ambao mpaka sasa unashikiliwa na bondia huyo hali inayopelekea kuupoteza baada ya kupatikana kwa bingwa kwenye pambano hilo kufuatia Gregor kushindwa kuutetea tangu mwaka 2016 kabla ya pambano lake na Floyd Mayweather Jr. mwezi Agosti mwaka  2017.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents