Burudani ya Michezo Live

Video: Tundaman kufungua shule ya muziki kusaidia wasanii wachanga

Msanii wa Tip Top Connection, Tundaman amesema anatarajia kufungua shule ya muziki itakayowasaidia wasanii wachanga nchini.

‘Sasa hivi nataka nifungue shule ya undergrounds,” Tunda aliiambia Bongo5. “Ni shule ambayo kiukweli itakuwa inatoa vipaji tu vya kucheza pamoja na kuimba. Nshapata eneo kule Tabata naandaa madarasa.” Tunda amesema tayari ameongea na Profesa mmoja wa chuo kikuu atakayekuwa miongoni mwa walimu na kwamba atakuwa na walimu wenye ujuzi wa muziki.

Katika hatua nyingine Tundaman alielezea maaan ya wimbo wake Msambinungwa aliomshirikisha Ali Kiba.

“Msambinungwa ni pretender, ni mtu mmoja hivi miyeyusho miyeyusho, ni mtu mmoja sio mkweli, ni mtu mmoja Malaya, ni mtu mmoja mizinguo, ni mtu ambaye hana sifa za kibinadamu hata kidogo,” alisema. Alisema neno hilo ni mchanganyiko wa Kiswahili na Kiluguru ambalo mama yake alikuwa anapenda kulitumia zamani wakati yeye alipokuwa mtoto.

“Kwahiyo nimelikumbuka nimeona Msambinungwa ni jina ambalo naweza nikalitumia katika nyimbo na nikaleta slogan nyingine katika muziki wa Kitanzania na nashukuru mwenyezi Mungu ngoma imetoka na watanzania wameipokea vizuri.”

Msanii huyo wa Tip Top amesema amepanga kumtumia Agnes Masogange kwenye video ya wimbo huo itakayofanyika Kenya kwakuwa msichana huyo ana sifa za ‘Kisambinungwa’.”Nilichukua watu wenye sifa za kisambinungwa. Ali Kiba pia Msambinungwa ndio maana nimemshirikisha.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW