BurudaniUncategorized

Video: Ukiiga maisha ya Gigy Money ‘ItakuCost’ – Coyo

Msanii wa muziki kutoka Tetemesha Entertainment, Coyo amefunguka kuzungumzia mapokezi ya wimbo wake mpya ‘ItakuCost’ ambapo alifafanua kuwa wimbo huo ametaka kuwaelimsha vijana kuacha kuiga maisha ya watu mitandaoni.

Coyo ameiamba Bongo5 kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakiaribikiwa kutokana na kuiga baadhi ya vitu wanavyoviona mtandaoni.

“Mimi nyimbo zangu zote lazima ziwe na vitu muhimu, ielimishe, iburudishe pamoja na kukosoa kama inawezekana. Kwahiyo wakati auandaa huu wimbo nilitaka watanzania kuacha kuigaiga vitu ambavyo havina msingi mwisho wa siku vikakucost. Ishi maisha yako kama unataka kuiga life style ya mtu angalia kwanza jifunze kupitia watu wengine,” alisema Coyo.

Rapa huyo alidai vijana wengi katika mitandao ya kijamii wamekuwa makiiga maisha ya watu kama akina Gigy Money na kujikuta katika matatizo.

“Kuna watu wanaona fulani anavyopiga picha mbaya na kuziweka mtandaoni yale ndio maisha, ile ndio kiki, mtu akiona picha za Gigy anavyojiachia yale ndio maisha ya ustaa, kumbe sio ukiiga ukaingia unajikuja kwenye matatizo,” alisema Coyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents