Burudani

Video: Uliona jinsi Damian Soul alivyopoteza kwenye Maisha Superstar wiki hii?

Damian Soul na mentor wake AY walipoteza mbaya wiki hii kwenye shindano la Maisha Superstar la Maisha Magic.

Kutoka kwenye performance ya wimbo wake ‘Ni Penzi’ iliyompa kura chache wiki iliyotangulia, wiki hii Damian alithibitisha uwezo wake wa kubadilika baada ya kuimba wimbo wa mwalimu wa washiriki wa Maisha Superstar, Erick Wainaina ‘Nchi ya Kitu Kidogo’

Kilichomfanya atishe zaidi ni kubadilisha wimbo huo kuwa sebene na kurap kama wafanyavyo waimbaji wa bendi za dansi. Damian ndiye aliyepata kura nyingi zaidi wiki hii.

Naye mshiriki mwingine wa Tanzania, Myra ambaye mentor wake ni Shaa, alifanya vizuri pia kwa kufanya mash-up ya nyimbo za Beyonce Drunk in Love na Diva.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents