Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Video: Underground Z’bar afunguka kutafutwa na Alikiba, kisa?

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka visiwani Zanzibar, Baraka Abdalah amesema miongoni mwa wasanii aliowahi kuwaomba msaada ni Alikiba na alimkubalia kumsaidia kufikia malengo yake.

Hata hivyo kutokana na baadhi ya sababu walishindwa kufanya kolabo kitu ambacho hadi leo Alikiba amekuwa akimtafuta na kumuulizia.

“Nilishawahi kumuomba Alikiba msaada na akataka anisaidie tu sana na mpaka leo ananitafuta ananiuliza kwanini ile project yetu hajaendelea?”  NYGGA ameiambia Bongo5.

Alikiba ni msanii ambaye ni staa na anajitambua na ana heshima yake na anajitahidi kujiweka katika mtu asiye na skendo. Nilianza kujuana naye tangu siyo Alikiba katika ngoma ya Maria ambayo alishirikishwa, tukawa tunapeana free style tu” ameongeza.

Licha ya Alikiba ameongeza kuwa producer Lamar alitaka pia amsaidie na alishawahi kufanya kazi na Mandojo na Domo Kaya na anaamini akiendelea kufanya vizuri atapata msaada mkubwa zaidi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW