BurudaniVideos

Video: Ushauri aliopewa Rayvanny na Jason Derulo

“Alichonishauri ni vipi naweza kupenya katika soko la Marekani, aliniambi naimba vizuri Kiswahili ila tafuta namna ya kuweka kingereza katika mistari yako na jaribu kufanya nyimbo ambazo ni universal song. Usifanyi nyimbo kwa ajili tu ya Watanzania, fanya nyimbo ambazo Watanzania watapenda, na dunia itapenda,” huo ni ushauri aliopewa Rayvanny na Jason Derulo.

Rayvanny ambaye ameshinda tuzo ya BET ameiambia Bongo5 wakati akiwa Marekani kwa ajili ya ugawaji wa tuzo hizo, ndipo alipopata fursa ya kuzungumza na star huyo mkubwa Marekani na hitmaker wa song ‘Swalla’ na kushauriana mambo kadha wa kadha.

“Kwa hiyo mwisho wa siku unaongeza soko lako na wewe unapata maana ya kufanya muziki kwa maana utakuwa unapata faida kwa sababu ukiangalia soko la kule (Marekani) ni kubwa sana na wasanii wa kule wanapata faida sana na wanakuwa na maisha mazuri sana,” ameeleza na kuongeza.

“Hata wakati nilikuwa nafanya kwenye studio yake kule kuna ngoma nilikuwa nimefanya kwa Kiswahili yeye akaibadilisha akaniambia weka maneno ya kingereza,” amesema Rayvanny.

Pia ameongeza licha ya kukutana na Jason Derulo ambaye mwanzoni walikutana nchini Kenya, pia wamekutana na mastaa kama Fat Joe, Chris Brown, Lil Wayne, Karrueche, Amber Rose, Dj Khaled na Future.

Tazama video hapa chini.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents