Michezo

Video: Uvutaji shisha kumponza Sergio Aguero mbele ya Pep Guardiola 

Mshambuliaji wa Manchester City , Sergio Aguero huwenda akaingia matatani dhidi ya meneja wake, Pep Guardiola baada ya kusambaa kipande cha video kinacho muonyesha akivuta shisha akiwa sambamba na mrembo Lola Magnin.

Mwanamitindo, Lola Magnin mwenye umri wa miaka 18, hapo jana siku ya Jumapili ameposti kipande cha video kwenye mtandao wake wa Instagram inayomuonyesha akivuta shisha yeye na nyota huyo wa Argentina huku wakiwa wenye furaha.

Aguero was spotted in the video clip posted online by 18-year-old model Lola Magnin

Video hiyo imemuonyesha Aguero mwenye umri wa miaka 30 akivuta waziwazi shisha mbele ya kamera akiwa na mrembo huyo.

 

Aguero aliwahi kuhusisha kutoka kimapenzi na mrembo huyo lakini alikanusha tuhuma hizo akidai kuwa hatoki kimapenzi na mtu yoyote licha ya kukiri kumfahamu.

”Sitoki na mtu yoyote, namfahamu lakini haimaanishi kuwa ndiyo natoka nae kimapenzi,” Aguero aliwahi kusikika akisema hivyo siku za nyuma kabla ya tukio hilo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents