Aisee DSTV!

Video: Vijana wanne wa Kitanzania washinda MultiChoice Talent Factory  ya DStv

Kampuni ya DStv Tanzania imetangaza washindi wanne waliokidhi vigezo katika shindano la MultiChoice Talent Factory lililozinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka huu.

Program hiyo itawawezesha jumla ya vijana 60 kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika kuweza kupata mafunzo ya filamu kwa kipindi cha mwaka mmoja katika vituo vitatu tofauti kimoja wapo kikiwa nchini Kenya (Nairobi) ambapo vijana hao wataishi hapo hadi tarehe 01 ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Mchakato mzima wa kuwapata washindi hao umechukua takribani miezi miwili ambapo kwa hapa nyumbani Tanzania zaidi ya vijana 160 walituma maombi yao ya kushiriki na kupatikana wanne pekee waliyokidhi vigezo baada ya mchujo uliyofanyika tarehe 20 ya mwezi Julai mwaka huu jijini Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW