Burudani

Video: Vilio vyatawala mapokezi ya mwili wa Ivan Uganda

Ivan Ssemwanga aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘The Bosslady’ ambaye sasa ni mpenzi na mzazi mwenzake wa mwanamuziki wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnum’, atazikwa Jumanne hii nyumbani kwao Kayunga, Uganda.

Mwili wa mfanyabiashara huyo wa Uganda aliyefariki nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya moyo, umewasili Jumapili hii nchini Uganda ambako leo utafanyiwa ibada maalum ya wafu katika Kanisa la Namirembe siku ya Jumatatu.

Semwanga alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

https://youtu.be/A33vd5f5HRE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents