BurudaniVideos

Video: Wakazi atoa ‘diss track’ kwa Godzilla, ngoma ni Zillnass Zillnass

Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Godzilla na Wakazi katika mitandao ya kijamii, suala hilo limechukua sura mpya mara baada ya Wakazi kuamua kuingia studio na kutoa wimbo maalumu ‘Zillnass Zillnass’ (Clown Rapper)  kwa Godzilla.

Wakazi ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kufanya hivyo kama changamoto kwenye muziki, na juzi walipokutana kwenye radio station katika kuchanana Godzilla alikuwa mtu wa maneno mengi kitu ambacho hata mashabiki wake hawamuamini tena. Rapper huyo amesema anachofanya ni utamaduni wa watu wa Hip Hop badala ya kuweka maneno mengi kwenye vitu vingine, unarekodi unaweka hisia zako kwenye muziki.

“So hii ni Zilla track it about me attack him kwa form ya muziki coz Hip Hop ndio utamaduni wetu ulivyo, sidhani kama utakuwa na uwezo wa kureply. Track imekuwa produced na Q pale Chimbo Inc na video imeshutiwa na upcoming director mmoja mkali sana, jina lake ni Gruzzie perfect” amesema Wakazi.

Ameongeza kuwa msanii(emcee) yeyote ambaye anataka kumchana anaweza kufanya kama alivyofanya yeye kwa kuonyesha uwezo, ufundi na ustadi bila kumtukana mtu, na sio kwenda kuzungumza mambo mengine au kujigamba nina kitu fulani kwani wasanii wanatakiwa kutambiana kwa uwezo wa kimuziki na si vinginevyo.

Tazama video hiyo hapa chini.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents