Videos

Video: Wakuvanga aichapisha albam yake China, atoa somo la namna ya kuifanya sanaa kuwa biashara

Mchekeshaji maarufu wa kundi la Orijino Komedi, Wakuvanga ambaye ameingia kwenye muziki, amesema aliamua kuipeleka albam yake nchini China kwaajili ya uchapishaji. Ameiambia Bongo5 kuwa gharama zote za kuitengeneza albam hiyo zimetoka kwenye kampuni yake ya ‘Wakuvanga Entertainment.

“Nimekwenda China, nimeprint albam yangu mwenyewe, nimetafuta kampuni ya kuprint mimi mwenyewe, nimeidhamini mimi mwenyewe, yaani mwekezaji wa kwanza kwenye project yangu ilikuwa ni mimi mwenyewe,” amesema.

Ameongeza kuwa ameingia ubia na kampuni nyingine kufanya biashara hiyo ya muziki kwakuwa ni biashara kama biashara zingine. Amelitolea mfano wazo la biashara ya Juma Nature ya ndala na kusema huo ni mfano wa kuigwa.

“Nimesikia Juma Nature, mmoja wa wasanii ninao waheshimu kuwa anataka kuanza kuuza kanda mbili zake. Kwangu mimi si dhambi, mtu kama Juma Nature akiwa na kandambili zake watu wote wa TMK wakivaa kandambilli za Juma Nature, hiyo ndio biashara ya sanaa, ndio biashara wanayofanya wenzetu wakina Jay-Z na ndio maana hawana hata ugomvi na media kwasababu wao wenyewe wana uwezo wa kuuza talent zao.”

Wakuvanga ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake uitwao Kato, amesema kampuni yake inahusika na kuandaa matamasha na kusimamia kazi za wasanii lakini kwanza imeanza kusimamia kazi zake mwenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents