Habari

Video: Walimu wa Tanzania kwenda Afrika Kusini kufundisha Kiswahili

Rais John Magufuli amesema wamekubaliana na Rais Jacob Zuma kupeleka walimu kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufundisha Kiswahili kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu na pia shule nchini humo.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati wa hafla kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

“Lakini pia nimewakaribisha pia Afrika Kusini kuja kuchukua walimu wa Kiswahili hapa nchini, lakini pia tukasema tutapeleka walimu wa kufundisha Kiswahili kwa vyuo vikuu na shule za Afrika Kusini wakati wowote na yeye tumekubaliana na amesema yupo tayari,” alisema Rais Magufuli.

Video:

Rais Zuma amewasili nchini tangu jana usiku kwa ziara ya siku tatu kufuatia mualiko kutoka kwa Rais Magufuli.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents