Habari

Video: Wanaume wawili wa Mombasa wakubaliana kisheria kumuoa mwanamke mmoja

Wanaume wawili wa Kenya wamesaini makubaliano ya kumuoa mwanamke mmoja. Mwanamke huyo alikuwa na uhusiano kwa wakati mmoja na wanaume hao kwa miaka minne na amekataa kumchagua mmoja.

Makubaliano hayo yanawaruhusu wanaume hao, Sylvester Mwendwa na Elijah Kimani kuishi na mwanamke huyo nyumbani kwake na watamsaidia kuwalea watoto wawili alionao. Gazeti la Daily Nation limeandika kuwa Mwendwa na Kimani wamelazimika kukubaliana hivyo baada ya kubaini kuwa wote walikuwa na uhusiano na mwanamke huyo wa Mombasa.

Sehemu ya makubaliano hayo inasema: Mimi Sylvester Mwendwa na Bw Elija Kimani, tume- kubaliana yakuwa kuanzia leo hatutawahi kubishana wala kuoneana wivu kwa ajili tayari tumejuana na mke ambaye anaitwa Joyce Wamboi ambaye amesema hayuko tayari kupoteza penzi letu.”

“Kila mmoja ataheshimu siku aliyopangiwa. Tunakubaliana kupendana na kuishi kwa amani. Hakuna aliyetulazimisha kufikia makubaliano haya.”

Mwenda amesema wazazi wake wamempa baraka zote na sasa anajiandaa kutoa mahari. Mwanamke huyo ni mjane na ana watoto wawili.

Source: Daily Nation, NTV, BBC, K24

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents