Video: “Wasanii wa Tanzania wanajituma na wamewekeza kweli kwenye muziki, Wanapendwa Afrika Mashariki yote mfano Alikiba na Diamond” – Mzazi Willytuva

Mtangazaji wa kituo cha CITIZEN RADIO kutoka nchini Kenya pia anayeendesha kipindi cha #MAMBOMSETO @mzaziwillytuva amefunguka mengi sana kuhusu tasnia ya muziki kwa upande wa Afrika Mashariki.

Akiongea na Bongo5 @mzaziwillytuva amesema kuwa muziki wa Bongo Fleva unakubalika sana Kenya na nchi zingine kwa sababu wasanii wa Tz wanajituma na wamejitahidi kuwekeza kwa undani kwenye muziki wao.

Mbali na hilo pia amesema mfano kwa taifa kama Kenya wanapenda aina ya muziki unaoimbwa lakini kikubwa zaidi nyimbo za Tanzania zimepewa airtime sana kwa upande wa Kenya huenda pia ikachangia.

Amewatolea mfano wasanii kama @mwanafa @aytanzania @husseinmachozi100 @officialalikiba @diamondplatnumz na @mbosso_ ni miongoni mwa wasanii wanaopendwa sana Kenya na muziki wao umefanya vizuri sana.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW