Burudani

Video: Wasanii watua nyumbani kwa RC Makonda, RC atoa ahadi hii kuhusu Roma

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, wameahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili kupatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu wasiojulikana Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.

Alisema hayo akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.

Akiongea na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu hao wako wapi.

“Natoa pole kwa ndugu pamoja na marafiki, hakuna mtu ambaye anaweza kupotelewa na mtu akawa na furaha na bahati mbaya tunaangaika kujua wapi waliko. Nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwamba tunapopotelewa na ndugu zetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio wakati ya kuyarusha rusha maneno na kufika hatua tunapoteza ushahidi,” alisema RC Makonda.

Alisema tayari ameliagiza jeshi la polisi kufuatia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata ufumbuzi mapema huku akiahidi mpaka Jumapili hii watu wao watakuwa wamepatikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents