Video: Washiriki 16 kupambana katika European Youth Film Competition 2017

Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu kuzinduliwa kwa shindano la European Youth Film Competition 2017, liloandaliwa na Umoja wa Ulaya na washirika wake tokea nchi ya Uholanzi, Ubalozi wa Ufaransa, Alliance Francaise pamoja na British Council kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wametajwa majina ya washiriki 16 waliongia katika kinyanganyiro cha kuwania sh. milioni 15.

Majina hayo ya washiriki yametajwa leo na Mratibu wa shindano hilo kutoka Andreson Media, Ndugu. Musa Sakari katika ofisi za Ubalozi wa Uingereza huku hafla hiyo ikiudhuriwa na Balozi wa Uingereza Roeland Van De Geer, Afisa habari wa Umoja wa Ulaya, Susanne Mbise na Mr. Tairo kutoka Bodi ya filamu Tanzania.

Katika hotuba yake Balozi Van de Geer amesema kuwa ” Filamu hizo zilizochaguliwa mimekidhi ubora wa picha, ubunifu, zinaendana na mandhari pamoja na kufuata maelekezo ya shindano”.

Naye Bi Susanne aliwataka washiriki ambao hawajapita katika 16 bora wasikate tamaa bali watumie fursa waliopata kuonyesha uwezo wao katika sekta ya filamu.


Baadhi ya washiriki waliotoks katika shindano hilo

Wakati wa kutaja majina, Musa Sakari alieleza kuwa ” Filamu hizo zilizopita zitaweza kuonyeshwa katika maeneo ya Biafra tarehe 5/08/2017, Mbagala Zakiema tarehe 12/08/2017, Mwembe Yanga tarehe 19/08/2017 na Alliance Francaise tarhe 02/09/2017.”

Aliongezakuwa ” Lengo la kuonyesha filamu hizo hadharani ni kuwapatia nafasi watazamani kuchagua filamu bora kwao ambapo wataweza kupiga kura katika kipengele hicho cha People Choice kupitia ujumbe mfupi.”

Majina ya Washiriku 15 walofika fainali

1. Christine Pande- Jina la Filamu Msafiri Short Film

2. Cornel Mwakyanjala- Jina la Filamu Majanga- Animation

3. Daniel Leonard Manege-Jina la Filamu Turudi Nyumbani

4. Dennis Samuel Chacha – Jina la Filamu Home the hills

5. Dosi Said Dosi – Jina la Filamu Uharibifu

6. Florence Mkinga-Jina la Filamu Ngoma

7. Frances Joseph Nyerere – Jina la Filamu The Source

8. Frank Slyvester Machibya- Jina la Filamu Baraka

9. Freddy Shabani Feruzi -Jina la Filamu Bajaji

10. Karim Muhidin Michuzi -Jina la Filamu Urban Migration

11. Kherry Seleman Kafuku -Jina la Filamu Kijacho

12. Louis Shoo -Jina la Filamu Watoto Wangu

13. Malik Khatib Hamis -Jina la Filamu Clinic

14. Rashid Shaban Songoro -Jina la Filamu Tone

15. Tarangwa Anthony Marwa – Jina la Filamu Shida za uani

16.Wambura Nyigana Mwaikabe -Jina la Filamu Watu na Samaki

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW