Burudani

Video: Washriki TPF Waenda Kenya

Washiriki wa Tanzania katika kinyang’anyiro cha kusaka viapaji katika ukanda wa Afrika mashariki Tusker Project Fame wameondoka alfajiri ya jana kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya.

 

Washiriki hao ambao waliondoka majira ya saa kumi na moja alfajiri wanaungana na wenzao kumi na mbili kutoka nchini zingine nne za ukanda huu wa Afrika Mashariki ambapo watachuana kuwania mkataba wa kurekodi albamu katika studio za Gallo record nchini Africa kusini pamoja na zawadi ya shillingi millioni

Wakizungumza na Bongo5.com katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere washiriki haoJaneth Christopher, Aneth kushaba,Leah Mwambogela na Cynthia bavo ambaye alichelewa na nusura kuachwa na ndege walisema wana imani ya kurudi na ushindi katika shindano la mwaka huu na waliwataka watanzania kuwaunga mkono katika kampeni yao ya kusaka ushindi.

Aidha mshiriki Peter Msechu ameondoka leo asubuhi kuelekea jijini Nairobi kujiunga na wenzanke kabla ya kuanza kwa kambi hiyo rasmi siku ya kesho.

Usaili wa washiriki hao utaonyeshwa jumapili ya tarehe 26 katika Televisheni ya taifa TBC 1 kuanzia saa tatu usku na pia kutakuwa na mnuso wa uzinduzi wa shindano hilo ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kuwakaribisha wasiriki 3 ambao wamefuzu kuingia kwenye shjindano hilo kutoka katika nchi shiriki jumapili ya tarehe 10 ya mwezi wa kumi.

Bongo5 inawatakia washiriki hao wa Tanzania kila la keri katika kuliwakilisha taifa katika medani ya muziki.

{hwdvs-player}id=1167|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1166|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1165|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents