Habari

Video: Waziri mkuu wa UAE, Sheikh Mohammed aamuru ndege zisiruke wakati wa Interview yake na BBC kuepusha kelele

Waziri mkuu na makamu wa Rais wa United Arabs Emirate (UAE) Sheikh Mohammed, hivi karibuni alifanyiwa mahojiano na kituo cha runinga cha Uingereza BBC huko Dubai.

dubai prince

Akielezea jinsi ilivyokuwa kabla ya interview hiyo, mtangazaji wa BBC Jon Sopel, amesema baada ya kupewa ruhusa ya kufanya naye mahojiano walifika eneo la kufanya Interview kama walivyoahidiwa.

Kwa mujibu wa Jon, sheikh mohammed kwa kawaida huwa hafanyi mahojiano mara kwa mara, na wakiwa katika eneo ambalo walipanga kufanyia Interview hiyo Camera man wa BBC aligundua kuwa kuna kelele nyingi za ndege (aircraft) zinazopita katika anga la eneo hilo hivyo zingeleta shida wakati wa mahojiano.

mohd1301
Sheikh Mohammed na Jon Sopel wakati wa Interview

Ameendelea kusema walipouliza itakuwaje kuhusu kelele za injini za ndege hizo, watu wa sheikh mohammed waliwaambia hakuna tatizo hilo pia litawezekana kuzuia ndege hizo.

Jon amedai kuwa kesho yake walifanya interview vizuri na hakuna ndege hata moja iliyoruka wakati wote wa interview hadi mwisho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents