BurudaniVideos

Video: Witness awachana wanawake wasionyonyesha kuogopa maziwa kulala

Msanii Witness a.k.a Kibonge Mwepesi amewachana wanawake wasiopenda kunyonyesha pindi wanapojifungua kuhofia maziwa yao kulala.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Mzuka’, amesema suala hilo halina ukweli wowote na wanaponyonyesha wanajiepusha na mambo mengi.

“Kwenye maziwa kuna fat kwa maana ya mafuta wao wanaposema sinyonyeshi kwa sababu ziwa langu litalala ndipo wanapoharibu mfumo mzima wa shape zao lakini wanatakiwa wafahamu kuwa wanatakiwa kunyonyesha miezi sita,” Witness ameiambia Bongo5 na kuongeza.

“Faida zake utatengeneza mfumo mzuri kwa mtoto  na kujikinga na magonjwa, pia yeye mwenyewe inamsaidia kwa sababu mfumo wake wa mwili unarudi katika hali yake ya kawaida kwa sababu vile virutubisho vyote vilitengenezwa kwa ajili ya mtoto, sasa ukiviacha ndio unakuta matinginya mtu anakuwa na mwili mbaya lakini mwisho wa siku watu nyonyosheni,” amesema Witness.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents