BurudaniVideos

Video: Wizkid aeleza namna alivyokuzwa na baba muislamu na mama mlokole katika familia yenye watoto wa kike 7

Wizkid amekuwa katika mazingira tofauti na watu wengi. Baba yake ni muislamu, mama yake ni mlokole.

“Siwezi kubadilisha kitu hicho,” muimbaji huyo wa Come Closer amesema kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Channel 4 News ya Uingereza.

“Kwasababu hicho ni kitu ambacho kimenisaidia katika kuwa nilivyo leo, kuishi kwenye nyumba ambayo mama yangu ni Mkristo na baba yangu Muislamu na hakuna hata siku moja wamelumbana kuhusu dini au wanachotaka kufanya watoto kwasababu baba yangu alikuwa anasema ‘fanya chochote unachotaka, kama unataka kuwa muislamu sawa, nenda kanisani au nenda msikitini, fanya chochote unachotaka.’ Kile nilichoelewa ni kuwa upendo ulikuwa kitu pekee kilichowafanya wawe pamoja kwa muda mrefu sana. Wazazi wangu wamekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu sana, dada yangu mkubwa ana kama miaka 38, wazazi wangu wamekuwa pamoja katika unene na wembamba,” alieleza.

“Hiyo imesaidia katika namna niyaonavyo maisha, kusambaza upendo zaidi, na nawapenda wazazi wangu hadi kufa, nawapenda mno, ni kila kitu kwangu.”

Wizkid amedai kuwa haikuwa rahisi kwa wazazi wake kuamini kama muziki unaweza kuwa kitu cha muhimu kwake hasa ukizingatia kuwa alikuwa msanii wa kwanza mwenye umri mdogo Nigeria kufanikiwa kwa ukubwa huo.

“Wazazi wangu hawakuamini kuwa kulikuwa na nafasi katika hiyo, walisema ‘baki shuleni, hatutaki uende studio na baba yangu alikuwa akinigombeza kila mara ‘usiende studio, kaa nyumbani, soma.’ Lakini nilikuwa na ndoto zangu nilizozifuata, nilihitaji kuwashawishi kufanya vizuri darasani, kufanya show zangu na kuhakikisha wanaona kutoka nje, watu waliwaambia ‘mmemuona mtoto wenu, ameenda kwenye show mbele ya watu elfu 40 na baba yangu akawa ‘labda yuko serious.’”

Kwa upande mwingine Wizkid amedai kuwa kuzaliwa kwenye familia yenye watoto saba wa kike kumemfanya awaelewe zaidi wanawake.

“Nahisi kama nawajua wanawake sana, ninapokaa na kuzungumza na msichana nahisi kuwa naweza kugusu sehemu yako ya ndani,” anamuambia mtangazaji wa kike aliyemhoji.

“Ni sababu nimekua kwa kuzungukwa na dada saba. Nimewaona wakigombana leo ‘sitazungumza na mwanaume huyu’ na kesho wanafurahi na jamaa, hiyo imenifanya niwaelewe wanawake, na wanawake ni watu special na nina marafiki wengi wa kike kuliko wa kiume.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents