Moto Hauzimwi

Video: Wolper ni msichana mzuri akiniambia ananipenda sawa – Msamii

Msanii wa muzki wa Bongo Flava , Msamii amemwagia sifa muigizaji wa filamu Bongo, Jackiline Wolper na kudai kuwa akiambiwa anapenda na muigizaji huyo basi hato vunga.

Akiongea na Bongo5, Msamii amedai kuwa hamfahamu kabisa mwanaume anayeitwa Brown anayedaiwa kutoka kimapenzi na mrembo huyo bali anamfahamu ex wake wa WCB Harmonize.

“Simfahamu Brown namjua Wolper,” amesema msanii huyo ambaye akaongeza kuwa ” Mimi najua kuhusiana na Harmonize tu.”

“Wolper ni msichana mzuri akiniambia ananipenda why not, Mimi sipendi mambo ya kutumia ma-DM nini yani kama nampenda nitamfuata tu moja kwa moja kwa sababu najua anapopatikana na yeye kama ananipenda atanifuata mambo ya DM ya nini tena,” amesema Msami.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW