Tupo Nawe

Video ya AY na Diamond ‘Zigo’ remix yapata views zaidi ya milioni 1 ndani ya wiki 1

Miongoni mwa vipimo vya video ya muziki kupokelewa vizuri ni pamoja na namba za watu waliotazama au kupakua mtandani. Kwa kutumia kigezo hicho video ya wimbo wa AY aliomshirikisha Diamond imeonesha mafanikio makubwa ndani ya siku kumi tu.

AY na Diamond

Video hiyo ambayo imefanyika Afrika Kusini na kuongozwa na kampuni ya Studio Space Pictures, iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube Ijumaa ya January 22 imefikisha watazamaji 1,201,819 hadi leo (Feb 1).

Speed hii inaweza kuifikisha mbali zaidi video hii ambayo ilianza kuonesha mafanikio makubwa ndani ya siku nne tu toka ilipotoka kwa kufikisha views laki nne na nusu na kuifanya kuwa video ya AY iliyotazamwa zaidi kati ya video zake zote.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW