Burudani

Video ya Ferooz yafunga mtaa Temeke

Feroozi_video_face
Jana mwanamuziki Feroozi Mrisho alikuwa akikamilisha video ya wimbo wake mpya ya Mnanda aliomshirikisha mwanadada kutoka THT, Shaz B. Video hiyo imefanyika chini ya mkono wa Adamu Juma wa Visual rab, maeneo ya Temeke.


Video hiyo iliweza kukusanya watu wengi na kufanya Adam kuwa na kazi ya ziada kupenya kwapani kwa watu ili kuweza kupata picha mzuri na Clear.
Feroozi_Video_watu_kibao
Hapa njia ilifungwa kabisa, Adam akiwa amesimama akijiuliza jinsi ya kuchukua picha za hapo.
Feroozi_video_wachafu
Hapa ilikuwa zamu ya mmoja mmoja au kundi kwa kundi…
Feroozi_video_ngongoti
He!! Ngongoti nao walikuwepo?  Na wao walionyesha mambo yao ya kucheza juu juu mchezo ambao kwa sasa unapotea pole pole kama ulivyopotea mchezo wa ‘ Super Power Ngeta Kibongee…’ na mchezo wa Mazingaombwe mashuleni..
Feroozi_video_muhogo

Muogo mchungu naye alikuwepo kwenye burudani hiyo, hapa alikuwa akiserebuka na Bi Mkubwa..
Feroozi_video_babu
Babuuuu!! akiwa na Emmy wakijitoa kimasomaso
Feroozi_temba_chege

Kweli hii ilikuwa kali… Masawe aka Temba yeye alikuwa upande wa Ngoma pamoja na mtoto wa mama Saidi aka Chege Chigunda, katika Muhogo mchungu akijiuliza aanza kucheza ngoma ya nani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents