Tupo Nawe

Video ya Lava Lava ya Shaa imefanyika Morogoro

Kama umeitazama video ya wimbo mpya wa Shaa uitwao ‘Lava Lava’ bila shaka utakuwa unajiuliza hiyo milima inayoonekana humo ni ya wapi! Well jibu ni kuwa video hiyo imefanyika mkoani Morogoro.

http://www.youtube.com/watch?v=n68rQ3890u0

Akiongea na Clouds FM kwenye kipindi cha XXL, Shaa amesema yeye, muongozaji wa video hiyo, Adam Juma, madansa na crew nzima walifunga safari kuelekea mkoani humo ili kupata maeneo yatakayoendana na wazo walilokuwa nalo awali.

Shaa ambaye jina lake halisi ni Sarah Kaisi amesema wakati wanaukaribia mji wa Morogoro, waliona location nzuri barabarani na kuamua kusimama hapo kuanza kazi hiyo. Amesema walishoot video hiyo mpaka usiku wa saa sita ambapo yeye na madansa wake walipata michubuko ya hapa na pale kutokana na mawe kwenye milima hiyo.

Kuhusu gharama ya video hiyo, Shaa amesema imetumia karibu shilingi milioni 6.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW