Video ya Mulugo kwenye Youtube yaangaliwa mara 7,000+ ndani ya saa 24

Video ya naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mheshimiwa Philipo Mulugo katika kongamano la elimu nchini Afrika Kusini ambayo imekuwa gumzo kwa jinsi alivyosema Zimbabwe ni kisiwa kimoja wapo kilichounda Muungano wa Tanzania, imeangaliwa kwa zaidi ya mara 8,000 ndani ya saa 24.

Video hiyo imejipatia umaarufu zaidi jana licha ya kuwepo tangu October 18, baada ya vyombo vya habari hususan Clouds FM kuishikilia bango na kucheza kipande hicho mara nyingi siku ya jana.

Asubuhi ya jana wakati tunaitazama video hii Youtube, ilikuwa na views 8,000 na kitu lakini mpaka sasa video hiyo imeshangaliwa kwa zaidi ya mara 15,000.

Leo kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM kimemhoji naibu waziri huyo na kujitetea kuwa hayo ni makosa ya kawaida.

“Kuna aina tatu ya kusoma miaka unaweza ukasoma kwamba one,nine sixty four au wengine mpaka wanasema twenty zero seven au mwingine anasema two ,zero,zero,nine na mimi pale nia yangu nilikuwa nataka kusema digit moja moja sasa nilipotaka kusema digit moja nikashtukia nime sema digital mbili tena. Kwahiyo ni vitu ambavyo ndiyo maana nimesema havijakaa very grammatical kwamba nimekosea Kiingereza kama watu wanavyo ipanua kwa mfumo huo lakini kama watu wamenielewa hivyo basi niombe tu msamaha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents