Diamond Platnumz

Video ya ‘My Number 1′ ya Diamond Platnumz imetazamwa mara 971,235 ndani ya miezi miwili toka iwekwe Youtube

Ni dhahiri kuwa jina la Diamond Platnumz linazidi kukua, kutoka Tanzania hadi Afrika mashariki na sasa Afrika magharibi baada ya kufanya collabo na Davido ambayo bado haijatoka, hii yote inasababisha watu wanaofuatilia kazi zake na kila anachokifanya wazidi kuongezeka.

Kupata views nyingi katika mtandao wa video Youtube kwa msanii hutegemea vitu kadhaa ikiwa ni pamoja na ukubwa wa msanii, umaarufu wake pamoja na uzuri wa video unaoweza kusababisha watu wengi waitafute.

Video mpya ya hit single ya sasa ya Platnumz ‘My Number One’ ambayo ilipandishwa Youtube September 2 kupitia Channel ya Diamond Platnumz, mpaka leo November 6 imetazamwa mara 971,125 ikiwa ni miezi miwili tu toka ipandishwe.

Video ya ‘Nataka kulewa’ iliyowekwa youtube miezi 11 iliyopita imetazamwa mara 101,401 na ‘Kesho’ iliyowekwa miezi 10 iliyopita imetazamwa mara 270,901.

Ikumbukwe kuwa Diamond aliamua kuwekeza pesa nyingi kwaajili ya kwenda kufanya video ya ‘My Number One’ nchini Afrika Kusini, na hakuna ubishi kuwa uwekezaji wake umezaa matunda toka siku anaizindua video hiyo, kwa kumpa michongo mbalimbali ya kuingiza pesa kupitia ngoma hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents