Diamond Platnumz

Video Ya Nataka Kulewa Kuonekana Kwa Mara Ya Kwanza Jumapili

Poster ya Nataka kulewa Video.
Ile music video ya msanii Diamond Platnumz, ambao wimbo wake ulileta utata baina ya wasanii watatu, namaanisha H-Baba, Pasha na yeye Diamond, “Nataka kulewa” imekamilika na kilichobaki ni kuachiwa siku ya Jumapili ya wikiendi hii.
Kwa mujibu msanii Diamond na wa meneja wa msanii huyo Raqey ambaye ndiye alikuwa muongozaji mkuu wa utayarishaji wa video hiyo, kila kitu kimeshakamilika ikiwemo post production editing na sasa kilichobaki ni kuachiwa rasmi siku ya Jumapili katika Street Bash Party iliyoandaliwa na Clouds media kusherehekea kutimiza miaka 13 kwa kituo cha Radio ya Clouds FM.
Well, hatuna mengi ya kusema kwa kuwa yashasemwa sana tunachosubiria ni kuona kiwango chake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents