Burudani

Video ya Ommy Dimpoz ‘Wanjera’ yakamata namba 1 kwenye Top 10 ya SoundCity TV ya Nigeria

Muziki wa Bongo unazidi kupenya na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali barani Afrika.

Ommy2

Video ya Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz anayewania tuzo tuzo ya Afrimma mwaka huu katika kipengele cha ‘Best New Comer’, imeongezeka kwenye orodha ya video za wasanii wa Tanzania zilizoingia kwenye chart za vituo hivyo.

Ommy Soundcity

‘Wanjera’ imeshika nafasi ya 1 kwenye Top Ten East ya SoundCity TV ya Nigeria wiki iliyomalizika.

Wasanii wengine wa Tanzania ambao wamewahi kufanya vizuri kwenye chart hiyo ni pamoja na Diamond, Vanessa Mdee, AY, Jux, Navy Kenzo na Yamoto Band na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents