Burudani

Video ya ‘Sophia’ ya Ben Pol yavunja rekodi ya video zake zote

Muimbaji wa R&B Benard “Ben Pol” Paul ana sababu nyingi za kufurahia mafanikio anayoendelea kuyapata kupitia wimbo wake wa ‘Sophia’ ambao pia umekamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Marimba ya wiki iliyopita. Baada ya kuachia video ya wimbo huo iliyofanyika nyumbani kwao Dodoma, video hiyo imeweka rekodi mpya katika historia ya video zake alizowahi kutoa.

Video ya ‘Sophia’ iliyoongozwa na Khalfani imefikisha views 54,271 kwa siku tatu toka ilipowekwa rasmi kwenye mtandao wa YouTube.

“Sophia imevunja rekodi, yaani sijawahi kuwa na video ambayo imefikisha views 54,000 ndani ya siku tatu, haijawahi kutokea.” Ben Pol ameiambia Bongo5.

“Video kubwa kabisa ina views kama laki moja na nusu ambayo ni ‘Jikubali’, lakini Jikubali sasa hivi ina kama miaka miwili” aliongeza Ben Pol.

Ben Pol ametoa sababu anazohisi kuwa zimechangia watu wengi kutaka kuitazama video hiyo toka siku ilipotoka.

“Hisia zangu mimi zinaniambia kwamba watu nadhani waliisubiri kwa hamu, walikuwa wananiuliza sana kwenye social media Ben video ya Sophia lini, hiyo moja halafu cha pili kufanya video na video vixen mwenye albinism nadhani na yenyewe imesaidia sana. Watu wengi labda walikuwa wakiambiwa wanataka waione, kwahiyo mtu akimwambia mwenzake naye anataka kuona kama ni kweli Ben Pol amecheza na msichana mwenye ulemavu wa ngozi, na wamecheza chezaje anafananaje, kwahiyo hiyo pia imechangia sana watu kutaka kujionea wenyewe kile wanachoambiwa.” Alisema Ben.

Video ya ‘Jikubali’ iliyowekwa YouTube Jun 10, 2013 mpaka sasa ina views 153,416, ‘Unanichora’ iliyowekwa Jun 27, 2014 ina views 100,435 na ‘Sophia’ iliyowekwa Apr 20, 2015 ina views 54,271.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents