Habari

Video: Yaliyojiri bungeni Dodoma Leo

Leo Jumatatu Bunge limeendelea na mkutano wake wa tatu kwa wabunge kuuliza maswali kwenye wizara husika na kujibiwa hapo hapo. Tazama kilichoendelea Bungeni.

Mhe.Dt. Mary Nagu aililia seriakli juu ya upungufu wa watumishi wa afya pamoja na vifaa tiba katika wilaya ya Hanang.

Mbunge wa Korogwe mjini Mhe.Chatanda aihoji serikali juu ya kuunganisha mji wa Korogwe na viunga vyake katika gridi ya taifa.

Mhe.Makilagi aibana wizara ya fedha juu ya ucheleweshaji wa fedha za miradi ya maendeleo kutotolewa kwa wakati kwa wananchi.

Mh. Jafo akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Mhe.Kemilembe kuhusiana na ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya Sekouture

Mh.Marwa mbunge wa Serengeti asimamia kidete ujenzi wa miundombinu katika hifadhi ya mbuga ya Serengeti.

Mhe. Masala aitaka serikali kueleza hatma ya tafiti za madini zinazofanywa na makampuni tofautitofauti wilayani Nachingwea.

Mh.Ester Matiko aitaka serikali kutoa maelezo ya kina juu ya wananchi wa kata za Tarime ambao hawakulipwa fidia za ardhi yao.

Suala la wananchi wanaougua ugonjwa wa saratani kuchelewa kupatiwa huduma katika hospitali ya Ocean Road laibuliwa bungeni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents