Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Video: Yanga imezaliwa kwaajili ya mataji – Dismas Ten

By  | 

Msemaji wa mabingwa wa kihistoria ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Dar es salaam Young Africans, Dismas Ten amesema kuwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya hasimu wao Simba SC ni wa muhimu kwao kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa kombe la Vodacom kwa mara ya nne mfululizo.

Ten ameyasema hayo alipo hojiwa na Bongo5 kuelekea mchezo wao wa hapo kesho.
“Mchezo ni muhimu kwa sababu sisi tunahitaji kushinda ilikuendeleza rekodi yetu, Yanga SC imezaliwa kwaajili ya mataji na kushinda michezo”,amesema Ten.

Dismas Ten ameongeza kuwa “Kwa hiyo sisi tunahitaji kushinda ili kutengeneza mazingira mazuri ya kutwaa ligi msimu unaokuja kwa sababu tunahitaji kuweka historia ya kuchukua mataji mara ya nne mfululizo”.

“Ngao ya Jamii ni muhimu na sisi tunaitazama kwa kuhitaji kushinda sababu ni mabingwa mara 27 hivyo tumejiandaa pia kushinda msimu ujao timu yetu ipovizuri hakuna shaka yoyote wana Yanga wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao” alisema msemaji huyo wa Yanga Dismas Ten.

By Hamza Fumo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW