Michezo

Video: Yanga pamoja wanatoka Giningi uchawi hautosaidia kesho – Haji Manara

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa mchezo wa kesho wa Ngao ya Hisani dhidi ya Dar es salaam Young  Africans wataibuka na ushindi mnono licha akidai kuwa watani wao wa jadi wanatokea Giningi na hivyo akisemakuwa kama uchawi ungekuwa unasaidia timu ya taifa ya Congo ya mwaka 1974 wangeibuka na ushindi Wolrd Cup dhidi ya Yugoslavia licha ya kubeba wanga ndege nzima.

Haji S Manara ameyasema hayo leo hii alipozungumza na Bongo5

“Mchezo wa kesho Simba SC tupo tayari kwaajili ya vita, Yanga wamesajili vizuri na wanawachezaji wenye uzoefu wa Derby lakini nadhani sisi tupo vyema  zaidi yao”, amesema Manara.

Msemaji huyo  wa Simba  SC ameongeza kuwa  “Matarajio yetu ni kushinda kesho na kuchukua Ngao ya Hisani tunawaomba waamuzi  wachezeshe kwa kufuata  kanuni 17 za mchezo ili mshindi halali apatikane tumejiandaa kwelikweli na tumejipanga kwa sababu mchezo huu unahusisha zaidi ya ushabiki wa kawaida kwa sababu unaamua hatima ya myoyo ya watu, Yanga hawezi kuchomoka kesho idadi ya magoli hatujui”.

“Wenzetu wanacheza na akili za watu yakwamba wanatoka Giningi wanatoka wapi haisaidi mpira na mambo ya uchawi wangeshinda Congo ya Zaire 1974 walikwenda Wolrd Cup wakiwa na ndege nzima iliyojaa wanga wakachukua tisa kwa timu ya taifa ya Yugoslavia ni hisabu zaidi za uwanjani”.

“Tutawaheshimu sana Yanga kama watakuja kesho bila visingizio maana wameshaanza mchezo wa mpira ni mchezo wamakosa chochote kinaweza kutokea”, alimalizia Haji Manara.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents