Michezo

Video: Yanga SC hii hatari yatinga kwa Producer Lamar, kuibuka na wimbo rasmi wa klabu

Klabu kongwe kuliko zote hapa nchini, Yanga SC ipo katika mipango ya kutengeneza wimbo wake rasmi utakao kuwa unatumika na mashabiki na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi.

 

Kupitia ukurasa wake wakijamii wa Instagram Yanga SC imeeleza nia hiyo na tayari hatua zimeshaanza kufuatwa baada ya kufika katika studio za mkali wa kutengeneza mziki wa Bongo fleva, Lamar na kuanza kutengeneza biti.

Kwenye Studio za FishCrab na ‘Prodyuza’ bora wa Bongo Fleva @lamarfishcrab_ Matayarisho ya wimbo wa klabu @yangasc (official club Anthem) yameanza..! Hapa tukijaribu kujifunza kutoka wimbo wa #GGMU.
Kama unajua wewe ni mkali wa kuandika mashairi cheki nasi kwa [email protected] #thebigteam

Gwiji wazamani wa muziki raia wa DR Congo, Pepe Kalle aliwahi kuiyandikia klabu hiyo wimbo uliyofahamika kama ‘Yanga Afrika’ na kupata umaarufu mkubwa ndani ya baraza zima la Afrika.

Pepe Kale ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kufariki kwa ugonjwa wa moyo Novemba 1998 aliituntungia Yanga SC wimbo huo baada ya klabu hiyo kubeba taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kagame) Uganda mwaka 1993, akipewa tenda hiyo na aliyekuwa mfadhili mkuu marehemu Abbas Gulamali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents