Michezo

Video: Zlatan ageuza ligi ya Marekani uwanja wa ngumi

Japo umri umeonekana kuwa mkubwa kwa Zlatan Ibrahimovic lakini bado hajaacha utukutu wake hata kidogo. Mchezaji huyo jana alijikuta akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kibao mchezaji mwenzake.

Tukio hilo lilitokea wakati LA Galaxy ilipokuwa ugenini ikicheza na Montreal Impact kwenye mchezo wa ligi kuu ya Marekani uliochezwa kwenye uwanja wa Saputo.

Zlatan alifanya tukio hilo kwenye dakika ya 40 ya mchezo huo baada ya mchezaji wa Montreal, Michael Petrasso, kumkanyaga kwenye mguu wake wa kulia ndipo alipochukua maamuzi ya kumpiga kibao hiko.

Hata hivyo Galaxy waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililfungwa na Ola Kamara dakika ya 75.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents