Burudani ya Michezo Live

Video/Picha: ITV & Radio One kudondosha ‘Full Doze Concert’

Kituo cha runinga ITV, Radio na Capital Radio wamezindua rasmi Tamasha lao ”Full Doze Concert’ ambalo litakutanisha wasanii kibao wakali wa Bongo Flava, Singeli na Muziki wa Dansi.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo August 25, 2017, Dj Nicotrack ambaye anatangaza kipindi cha Dj Show cha Radio One amesema vituo hivyo vimekuwa vikifanya vizuri katika kutoa habari, mambo ya kijamii na burudani ila sasa wanataka kufika mbali zaidi kwa kuwaletea wasikilizaji na watazamaji wao pamoja na mashabiki wa muziki tamasha hilo la kukata na shoka.

“Tunasema Full Doze ni Burudani iliyojitosheleza na mlikuwa mkiipata kupitia TV na Radio zetu na sasa tunawaletea jukwaani kupitia Tamasha hili tunalotarajia kufanyika September 9 mwaka huu Dar Live Mbagala,” amesema Dj Nicotrack.

Tamasha hilo litakusanya wasanii wa Bongo Flava kama Beka Flavour, Juma Nature, Dully Sykes, Q Chillah na Snura, pia kutakuwa na live band toka kwa Banda ya African Stars (Twanga na Kupepeta) na upande wa muziki wa singeli atakuwepo Sholo Mwamba pamoja na ma-Dj wote kutoka vituo hivyo.

Picha zaidi

By Peter Akaro & Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW