BurudaniPicha

Video/Picha: Njemba lataka kubusu makalio ya Kim Kardashian hadharani, Paris

Duniani kuna mambo, tena ya ajabu kweli kweli. Na tena mengi yapo huko kwenye zile nchi wanazoziita za dunia ya kwanza – kuna vioja vya kukuacha mdomo wazi.

celebrity-pranker-vitalii-sediuk-strikes-again-this-time-grabbing-kim-kardashian-at-lavenue-restau-1
Vitalii alijipenyeza kwenye umati wengi wa watu kutaka kubusu makalio maarufu ya Kim Kardashian

Jumatano hii, njemba moja, tena maarufu, liitwalo Vitalii Sediuk lilifanya jambo la hatari,. Mchana kweupe tena katikati ya ulinzi mkali.. Kipi hicho? Lilitaka kubusu makalio ya Mrs Kanye West, Kim Kardashian.

celebrity-pranker-vitalii-sediuk-strikes-again-this-time-grabbing-kim-kardashian-at-lavenue-restau
Walinzi wa Kim Kardashian wakimzuia Vitalii kutotimiza azma yake

Mtu huyo ambaye amewahi kuwafanyia vimbwanga mastaa wengine, wakiwemo Brad Pitt na Leonardo DiCaprio, aliushika mguu wa Kim akitaka kubusu makalio yake lakini walinzi walimuwahi na kumbwaga chini.

kim-kardashian
Sasa unaelewa kwanini Kim Kardashian anahitaji walinzi wengi

Vitalii ametumia Instagram kueleza kwanini alifanya kioja hicho.

“I was protesting Kim for using fake butt implants. I encourage her and the rest of Kardashian clan to popularise natural beauty among teenage girls who follow and defend them blindly,” aliandika!

Inasemekana kuwa Kim amefungua mashtaka dhidi yake.

https://www.youtube.com/watch?v=caaQrWx0F9g

Tukio hilo limekuja wiki moja tu baada ya jamaa huyo huyo kumvamia mrembo Gigi Hadid kwa kumbeba juu juu huko Milan lakini akaambua bonge la kipepsi toka kwa mrembo huyo.

kim-kardashian-gets-attacked-by-vitali-klitschko
Pamoja na kufanya kitendo hicho cha hatari, Vitalii aliendelea kudunda mtaani

Pamoja na kufanya yote hayo Vitalii hajachukuliwa hatua na yupo uraiani akidunda kama kawa!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents