Burudani

Video/Picha: Roma atoa msaada na kufundisha shule ya msingi Mchikichini

Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki Alhamisi hii ametembelea shule ya msingi Mchikichini Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam na kutoa msaada wa vitabu vya hesabu pamoja na kuzungumza na wanafunzi katika namna ya kuwatia moyo kupenda somo la hisabati.

Rapa huyo ambaye alikuwa mwalimu wa sekondani hapo zamani, baada ya kusalimiana na mkuu wa shule hiyo, aliingia darasani na kufundisha somo la hisabati kwa wanafunzi wa darasa la saba pamoja na kuwapa mazoezi.

Akiongea na waandishi wa habari muda mchache baada ya kufundisha, Roma alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuwatia moyo wanafunzi kuhusu somo la hisabati.

“Nimekuja kutoa kidogo nilichonacho kwa sababu najua somo la hisabati ni changamoto kwa wanafunzi wengi. Kwahiyo nimetoa vitabu pamoja na kuwapa moyo wanafunzi juu ya masomo ya sayansi kwa sababu tukianza kuwajenga hapa kwamba hisabati sio ngumu wanakuwa nazo. Najua nilichokitoa sio kitu kikubwa sana lakini baada ya mimi kuna wasanii pamoja na wadau mbalimbali watafika hapa kuja kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimezungumzwa hapa,” alisema Roma.

Rapa huyo ameahidi kuendelea kutoa msaada wa namna hiyo katika shule mbalimbali ili kuinua ufauli wa wanafunzi katika masomo ya hisabati hasahasa shule za msingi.


Roma akiwa darasani na wanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Mchikichini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents