Burudani

Videos: Finalists wa EBSS wakiomba kura za mashabiki

Washiriki watano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano la Epiq Bongo Star Search wamesema wako tayari kwa ajili ya fainali inayotarajiwa kufanyika leo usiku katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall.

Wakiongea mbele ya waandishi wa habari jana jijini washiriki hao kila mmoja alijinadi kwamba amejiandaa vizuri na leo itakuwa siku ya kuthibitisha rasmi nani ni mkali kuliko wote watano kwani mshindi atafanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi za kitanzania milion 50.

Washiriki walioingia 5 bora ni pamoja na Walter Chilambo, Salma Yusuf, Nsami Nkwabi, Nshoma Nghangasamala na Wababa ambao wote wamekuwa kambini katika academy ya shindano hilo kwa mwezi mmoja sasa.
Ticketi zinapatikana Zizzou Fashions maduka yote, Shear Illusion, Best Bite, Maduka yote ya Robby One, Diamond Jubilee Hall na Katika ofisi za Benchmark zilizoko kawe. Kiingilio ni 10,000, 30,000 na 70,000.

Bongo5 itakujuza nini kimejiri leo siku ya fainali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents