Burudani

Videos: Jinsi Walter Chilambo alivyoibuka mshindi wa EBSS 2012

Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 kutoka Dar-es-Salaam Walter Chilambo usiku wa kuamkia Jumamosi amekuwa mshindi wa jumla wa shindano hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi za kitanzania Milioni 50 kama zawadi ya mshindi wa kwanza.

Walter aliibuka kidedea mbele ya Salma Yusuf kutoka Zanzibar ambaye walifaikiwa kuingia naye pamoja fainali ya washiriki wawili tu kati ya watano ambao walianza fainali hiyo hapo awali. Walter ambaye dalili za ushindi wake zilianza kuonekana tangu awali mwa fainali hiyo ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kujinyakulia kitita kikubwa katika mashindano ya kusaka vipaji vya muziki.

Aidha katika shindano hilo la kuamkia leo mshiriki Walter pamoja na wenzake walipitia hatua tatu ambapo ya kwanza ilikuwa kuimba na msanii mmoja mmoja waliowachagua ambapo yeye aliimba na msanii Ditto kabla ya kuimba mwenyewe katika raundi mbili zilizofuatia huku wakipigiwa kura na mashabiki katika raundi zote. Walter alitumia nyimbo moja ya Steve R n B “One Love”, na Nikikupata ya Ben Pol katika raundi zote mbili zilizofuata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents