Habari

Videos: Sababu za mgomo chuo kikuu cha Tumaini tawi la Dar es Salaam

Hapo jana kulitokea mgomo katika chuo kikuu cha Tumaini, Makumira Dar es Salaam ambao ulisababishwa na kucheleweshwa kwa fedha za mkopo kwa wanafunzi hao hali inayowafanya waishi wa shida.

Bongo5 ilikuwa katika eneo la tukio na kuongea na makamu wa Rais wa chuo hicho Jackson Shumbi aliyesema, “chuo hiki kama unavyo kiona kimekuwa na matatizo ya mara kwa mara, imekuwa siyo mara ya kwanza kama leo ilivyojitokeza na hii ni kwasababu ya record mbaya iliyo kwenye chuo hiki, migomo kama hii imekuwa ikitokea mara kwa mara wakati watu wakidai haki zao za msingi na hatimaye ukiangalia record ya nyuma imefikia muda watu wakipoteza masomo yao yaani kwa kufukuzwa chuo na hii ilitokea mwaka juzi, wanafunzi walifukuzwa na hatimaye wakawarudishwa mwaka huu, kwahiyo watatakiwa kumaliza mwaka unaofuata.”

Shumbi aliongeza kuwa migomo kama hiyo katika chuo hicho hutokana na sera ya ukandamizaji iliyo katika chuo hicho. “Kwasababu mimi ninachaoamini kwamba haki ya msingi anayo takiwa kupata mwanafunzi anatakiwa aipate kila wakati pale anapoiitaji kuipata, sasa inapotokea haki imekuja halafu inatokea mtu anaikandamiza either kwa maslahi binafsi, sisi wanafunzi lazima tu defend our right inapo tokea tunafanya vile.
Mimi naamini kitu kimoja kuna either wana maslahi binafsi ambayo wanayadefend sasa tunapo kuwa tunadai zile haki zetu either wanahisi tunataka kuwanyang’anya tonge ndiyo maana kunakuwa na tetesi either hizo fedha kutoka loan board maybe management inazifanyia biashara kwanza kabla ya kuziingiza kwenye akaunti za wanafunzi kwasababu haiwezekani fedha itoke mwezi wa 10 mwanzoni na leo ni mwezi wa 11 tarehe 8 fedha haijatoka mikononi mwa wanafunzi takribani mwezi mmoja kwahiyo kama mtu alifanya interest ya kuwekeza benki ili wazalishe hizo pesa halafu baadaye watupe kama refund ndiyo maana tunapoamua kustrike our own interest.”

Kwa upande wake mkuu wa chuo kikuu hicho amesema mpaka Jumanne ijayo fedha hizo zitakuwa tayari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents